JWTZ yatangaza nafasi za kujiunga na Jeshi kwa vijana wa Kitanzania

0
1

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza kuanza kwa zoezi la uandikishaji wa vijana wa Kitanzania kujiunga na jeshi, likilenga waliohitimu kuanzia kidato cha nne hadi elimu ya juu.

Tangazo hilo limetolewa Aprili 30, 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Gaudentius Ilonda, jijini Dodoma, ambapo alibainisha kuwa waombaji wote lazima wawe na kitambulisho cha taifa (NIDA), afya njema na wasiwe na rekodi ya kihalifu.

Vijana wanaotakiwa ni waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria au kwa mkataba wa kujitolea, awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo Cha Mafunzo au kikosi Cha kuzuia Magendo.

Kwa upande wa umri, waombaji wa elimu ya sekondari wanapaswa kuwa na umri usiozidi miaka 24, stashahada miaka 26, shahada miaka 27, huku madaktari bingwa wakiruhusiwa hadi miaka 35.

Aidha, taaluma adimu zinazohitajika ni Generall Surgeon, Orthopaedic Surgeon, Urologist Radiologist, ENT Specialist, Anaesthesiologist, Physician, Ophthalmologist, Paediatrician, Obstetrician & Gynaecologist, Ocologis, Pathologist, Psychiatrist, Emergency Medicine Specialist na Haematologist.

Pamoja na Medical Doctor, Dental Doctor, Veterinary Medicine, Bio Medical Engineer, Dental Laboratory Technician, Anaesthetic, Radiographer, Optometry, Physiotherapy na Aviation Doctor.

Taaluma za Uhandisi ni pamoja na Bachelor of Electronic Engineering, Bachelor of Mechanical Engineering, Bachelor in Marine Engineering, Bachelor in Marine transportation & Nautical Science, Bachelor in Mechanic in Marine Diesel Engine, Bachelor in Aviation Management, Bachelor in Aircraft Accident & Incident Investigation, Bachelor in Meteorology, Air Traffic Management & Aeronautic Engineering bila kusahau Fundi Mchundo Aluminum Welding na Welding & Metal Fabrication.

Kadhalika, maombi yaandikwe kwa mkono na yatumwe makao makuu ya JWTZ, Dodoma kuanzia Mei 1 hadi Mei 14, 2025, yakiwa na nyaraka zote muhimu kama cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kitaaluma, nakala ya kitambulisho cha taifa au namba ya NIDA, cheti cha JKT (kwa waliokihitimu), na namba ya simu ya mwombaji.