Kabudi na Mpango ndani ya baraza jipya la mawaziri

0
28

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli amefanya uteuzi wa mawaziri 2 katika baraza jipya la mawaziri.

Kwanza, amemteua Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Pili, amemteua Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Mawaziri Wateule hao walikuwa wakishikilia nyadhifa hizo katika Baraza la Mawaziri lililopita na uteuzi huu unaanza leo Novemba 13, 2020.

Send this to a friend