Kabudi: Tanzania inaheshimu uhuru na demokrasia

0
50

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amesema inasherehekea Miaka 60 ya Uhuru ikiendelea kuheshimu uhuru na demokrasia

Akizungumza katika mahafali ya 21 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Lushoto ameongeza kuwa Tanzania inaadhimisha miaka 60 ya uhuru ikiwa ni Taifa imara na siyo mkusanyiko wa makabila yasiyokuwa na umoja.

Amesema kuwa ndani ya miaka 60 ya uhuru Tanzania imeingia katika uchumi wa kati.  Amefafanua kuwa wakati wa uhuru, Tanganyika ilikuwa nchi maskini kuliko zote Afrika ya Mashariki na Kati, lakini leo ni nchi ya pili kwenye ukanda huo kuingia uchumi wa kati miaka mitano kabla ya wakati uliokuwa umetarajiwa, tena pamoja na kuwepo kwa ugonjwa wa UVIKO 19 uliosababisha uchumi kuporomoka kwenye mataifa mengi duniani.

“Tunasherehekea miaka 60 ya uhuru tukiwa ni taifa lililojikita katika kuenzi na kudumisha tunu za taifa ambazo ni amani, umoja, mshikamano, utu, haki, heshima, uhuru na demokrasia”, alisema Prof. Kabudi.

Ametaja mafanikio mengine makubwa ambayo nchi imeyapata katika kipindi cha miaka 60 ni kuwa taifa lenye udhubutu na moyo wa kujitegemea katika kufanya mambo makubwa kwa rasilimali zake yenyewe.

Send this to a friend