Kagame: Rais Samia ameleta suluhu ya kudumu ya migogoro

0
48

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na Rwanda zimekubaliana kuendelea kufanya kazi kwa pamoja katika masuala ya ulinzi na usalama ili kuhakikisha usalama katika nchi hizo mbili pamoja na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumpokea Rais wa Rwanda, Paul Kagame na ujumbe wake aliyewasili nchini leo Aprili 27, 2023 na kufanya mazungumzo ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.

Moja kati ya mambo yaliyozungumzwa ni pamoja na masuala ya biashara ambapo Tanzania inatazamia kuimarisha njia nyingine za mawasiliano ili iweze kutoa huduma kwa ufanisi nchini Rwanda na nchi nyingine, pamoja na kuimarisha bandari za Dar es Salaam na Tanga ambazo Rwanda wamekuwa wakizitumia.

“Tumeona haja ya kukuza biashara  na kuweka miundombinu ya kukuza biashara, kwa sababu kiwango cha biashara tulichonacho hakiendani na rasilimali tulizonazo kwa nchi mbili, lakini na uhusiano mzuri uliopo,” ameeleza  Rais Samia Suluhu.

Museveni akataa kusaini muswada wa mapenzi ya jinsia moja, aurudisha bungeni

Kwa upande wake Rais Paul Kagame amesema katika mazungumzo yao, wameazimia kujenga uchumi imara, siasa, utamaduni na uhusiano wa kihistoria ikiwa ni azma ya nchi zote mbili kuboresha maisha ya raia wake.

Mbali na hayo, Rais Kagame amemshukuru Rais Samia kwa kumwalika nchini pamoja na kusaidia kupata suluhu katika mgogoro Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku akieleza kuwa amani na utulivu ni hitaji muhimu  kwa ajili ya maendeleo na umoja wa Afrika.

Send this to a friend