Kaimu Balozi wa Marekani kuondoka nchini Tanzania

0
63

Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson anatarajia kuondoka nchini Tanzania hivi karibuni.

Patterson anaondoka baada ya kuuongoza ubalozi huo hapa nchini kwa kipindi cha miaka mitatu.

Katika salamu yake ya kuaga amewashukuru wale wote aliokutana nao na kufanya nao kazi hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuwaleta Watanzania pamoja na kuboresha maisha yao.

“Katika miaka hii mitatu, mimi na timu yangu ya ubalozi tumefanya kazi na wengi wenu kuimarisha mifumo ya nchi yenu ya afya na elimu. Tumewasaidia wakulima wenu hodari, tumesaidia kuwaandaa askari wenu majasiri kwa kazi zao za kulinda amani na kukuza utawala wa sheria,” amesema balozi huyo.

Amesifu uzuri wa Tanzania pamoja na ukarimu wa watu wake na kwamba atavienzi hivyo katika maisha yake yote.

Dkt. Patterson ni afisa wa masuala ya kigeni kitaaluma, na alianza utumishi wake nchini #Tanzania Juni 5, 2017 akichukua nafasi ya Balozi Mark Bradley Childress.

Send this to a friend