Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa atamrithi baba yake kama Rais ajaye nchini humo.
“Nitakuwa Rais wa nchi hii baada ya baba yangu. Wanaopingania mpango huu wamechelewa. MK Movement itashinda,” umesomeka ujumbe huo katika ukurasa wake.
Katika machapisho yake mengine yenye utata alibainisha kuwa kupanda kwake cheo cha juu nchini humo kuliandikwa kwa mawe na kujigamba kuwa hakuna ambaye angeweza kushindana naye.
Aidha, kabla ya chapisho lake Muhoozi katika ujumbe wake (ambao sasa umefutwa katika mtandao wa Twitter), alirejea tishio lake na Wakenya mtandaoni kuhusu mpango unaodaiwa kuivamia Kenya.
Wakenya wapika na kuuza chang’aa Uarabuni
Kulingana na Muhoozi, Wakenya wanahofia Uganda kwa sababu ya nguvu zake za kijeshi ambazo anadai ni bora zaidi kuliko za Nairobi.
“Wakenya wengine wanatuogopa kwa sababu wanajua jeshi letu ni kubwa kuliko lao. Jeshi letu linaweza kuikamata Nairobi baada ya wiki 1,” amesema Muhoozi.