
Jeshi la Polisi limesema linaendelea kumtafuta Augustino Polepole ambaye ni kaka wa Humphrey Polepole ili atoe maelezo yake na uthibitisho wa shutuma alizotoa dhidi ya Afisa wa Jeshi la Polisi aliyedai kuhusika na ‘utekaji’ wa Polepole.
Taarifa iliyotolewa na Polisi imeeleza kuwa Augustino anahitajika ili kuthibitisha kuwa, Humphrey Polepole alikuwa ni mpangaji ama mkazi wa nyumba aliyodai kuwa utekaji ulifanyika.
Hata hivyo, jeshi hilo limesema kuwa tayari limeanza uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa na Augustino kuhusu utekaji huo na kwamba jalada la uchunguzi lilifunguliwa mara baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo Oktoba 06, 2025.








