Kalemani: Kukata umeme hovyo kutamfukuzisha mtu kazi

0
72

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amelionya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuacha tabia ya kukata kata umeme hovyo.

Akizungumza na maafisa wa shirikka hilo mkoani Shinyanga Kalemani amesema kitendo cha kukata kata umeme hovyo tena bila taarifa hapendezwi nacho, na kubainisha tabia hiyo itakuja kumfukuzisha mtu kazi.

“Naombeni sana Mameja wa TANESCO nchi nzima acheni tabia ya kukata kata umeme hovyo, tena wakati mwingine bila hata kutoa taarifa ,fanye kazi zenu kwa ufanisi, na eneo ambalo halina umeme mna hatarisha usalama”, amesema Kalemani

Kuhusu ufanyaji kazi kwa mazoea amesema “fanyeni kazi zenu kwa ufanisi kama mlivyofanya kwenye miaka mitano iliyopita. Mlifanya kazi vizuri ya kusambaza nishati ya umeme kwenye maeneo mengi.”

Katika hatua nyingine, amewaonya watumishi hao kuacha kutoa lugha chafu kwa wateja, pamoja na kuacha kujihusisha kufanya kazi na vishoka, huku akitoa miezi mitatu ndani ya mkoa huo wananchi wote wawe wamesambaziwa huduma ya umeme.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mwandamizi Rasilimali wa TANESCO Makao Makuu, Festo Mkolla, amesema maagizo yote ambayo yametolewa watayafanyia kazi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa shirika hilo.

Send this to a friend