Kamanda aeleza mbinu zinazotumiwa na wanawake kuiba watoto Mwanza

0
52

Kutokana na matukio yaliyokithiri ya wizi wa watoto wadogo mkoani Mwanza, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa amefichua mbinu zinazotumiwa na wahalifu hao kuwa ni kujenga ukaribu na wazazi wa watoto hao ili kupata uaminifu wao.

Matukio hayo ya wizi wa watoto wa siku moja hadi miezi sita yameripotiwa mara kwa mara huku watuhumiwa wakiripotiwa kuwa ni wanawake wasioweza kupata watoto kutokana na ugumba.

“Mbinu zinazotumika kuiba watoto ni wanawake wenye nia ovu kuwa karibu na wazazi na kuaminiwa na kuachiwa watoto na hivyo kupata mwanya wa kutoroka nao,” amesema Kamanda Mutafungwa.

Serikali kufuatilia waliokamatwa na dhahabu India wakitokea Tanzania

Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na kutambua jukumu lao la msingi la kulea na kuwalinda watoto wao na kuacha uzembe wa kumwamini kila mtu.

Send this to a friend