Kamanda Muroto aeleza chanzo cha kifo cha Mwenyekiti wa BAWACHA aliyechomwa mshale

0
79

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (RPC), Gilles Muroto amesema chanzo cha kifo cha Mwenyekiti wa BAWACHA, Kata ya Palanga, Asia Said, aliyeuawa baada ya kuchomwa mshale usiku wa kuamkia leo ni ugomvi kati ya mume wake na mtuhumiwa wa tukio hilo, Haruna Ally.

Muroto amesema kuwa ugomvi huo ulisababishwa na mume wa marehemu, Hassan Masale, kuingiza mifugo kwenye shamba la alizeti la Haruna Ally.

“Tukio limetokea jana majira ya saa 2 usiku na alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Kondoa, na mshale uliotumika umekamatwa na mtuhumiwa amekamatwa na amekiri kufanya tukio hilo,” amesema Muroto.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa alikusudia kumchoma mshale mwanaume huyo lakini badala yake alimlenga Bi. Asia na kupelekea kifo chake.

Send this to a friend