Kamati: Chanzo cha uchafuzi Mto Mara ni tope lililotibuliwa na mvua

0
36

Uchunguzi wa kimaabara uliofanyika kwenye sampuli zilizochukuliwa katika maji ya Mto Mara umebainika kuwa chanzo kikuu cha kuchafuka kwa maji ya mto huo ni kusambaa kwa tope la uozo wa viumbe-vifu lililotibuliwa na mvua kubwa ilionyesha kwa kipindi cha muda mfupi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya kuchuguza chanzo cha kuchafuka kwa Mto Mara, Prof. Samweli Manyele akiwasilisha taarifa mbele ya waandishi wa habari.

Prof. Manyele amesema kuwa sababu kubwa ya kuchafuka kwa Mto Mara imetokana na mrundikano wa kiwango kikubwa cha tope lililosababishwa na uozo wa viumbe (organic matter) kilichobainika chini ya ardhi oevu ya huo.

Amevitaja viumbe hivyo ni pamoja na mimea ya matete, magugu maji na uwepo wa vinyesi vya wanyama uliosababishwa na wingi wa mifugo iliyopo katika eneo hilo.

Vilevile kamati imebaini kukosekana kwa hewa ya Oxygen katika maji ya Mto Mara hali iliyopelekea vifo vya Samaki na kusema kuwa hali hiyo imetokana na mmeng’enyo wa viumbe-vifu wakati wa uozeshwaji wake chini ya maji uliosababishwa na wingi wa mimea maji kwenye eneo oevu la Mto Mara.

Send this to a friend