Kamati: Uwezo mdogo kiakili chanzo wanafunzi kufeli Shule ya Sheria

0
35

Mwenyekiti wa kamati ya kufuatilia tathmini ya mafunzo yanayotolewa na taasisi ya uanasheria kwa vitendo nchini (LST) Dkt Harrison Mwakyembe, amekabidhi ripoti na kuainisha changamoto ambazo ni miongoni mwa vikwazo katika kupata wanafunzi bora wanaosomea fani ya sheria.

Kamati hiyo yenye wajumbe saba iliteuliwa Oktoba 12, mwaka huu na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, na kufanya kazi kwa siku 30 kufuatilia sakata la kufeli kwa wanafunzi wengi wa taasisi hiyo ya sheria.

“Uwezo mdogo wa wanafunzi wengi wanaoruhusiwa kusoma sheria na baadae kujiunga na Taasisi katika kumudu lugha ya kufundishia ya Kiingereza, tatizo hili lina athari kubwa sana katika uelewa wa masomo na kujieleza,” imeeleza taarifa ya kamati.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa changamoto nyingine ni kutokana na vyuo vingi vya sheria nchini kutozingatia masharti ya uwiano kati ya walimu na wanafunzi, sifa za waalimu, idadi yao na piramidi ya elimu.

Hata hivyo, kamati hiyo imesema changamoto nane zilizobainika ni za kimfumo na kisera na hivyo utatuzi wake hauna budi kuwa wa kimfumo na kisera

Send this to a friend