Kamati ya Bunge yashauri Barabara ya Kimara-Kibaha iwekewe tozo

0
51

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuanza na mfumo wa barabara zenye tozo katika mradi wa ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kimara mkoani Dar es Salaam hadi Kibaha mkoani Pwani ili kuongeza mapato.

Ushauri huo umetolewa wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipotembelea mradi wa barabara wa njia nane ambapo waliongozana na viongozi na watumishi kutoka TANROADS kuona maendeleo ya mradi huo ulipofikia pamoja na kuona changamoto zilizopo.

Akizungumza kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso amebainisha kuwa ujenzi huo ungeainisha barabara moja ya kulipia ambayo ingekuwa ikiipatia fedha Serikali na kutumika kwa ajili ya ukarabati.

Tahadhari yatolewa kwa wanawake wanaoweka tumbaku sehemu za siri

“Wajumbe hapa wameelezea umuhimu wa kuanza na barabara zenye tozo, mimi naamini kabisa kama tungekuwa tumejipanga kwa hizi hizi njia nane ni lazima tungekuwa na njia ambazo nyingine ni za kulipia, yaani barabara za tozo ili tuongeze mapato, duniani kote barabara nyingi zinajengwa kwa mfumo huu,” amesema.

Ameongeza kuwa “sheria inatukataza kujenga barabara za tozo kama hauna barabara mbadala, lakini hapa kuna njia mbadala kwanini msingelianza na hizi hapa tukawa na barabara za kulipia?”

Aidha, Kamati hiyo pia imeishauri Serikali kuanza kuufanyia kazi ushauri wa kulifanya Daraja la Tanzanite kuwa la tozo, na kila gari linalopita kwenye Daraja hilo lilipie fedha.

Send this to a friend