Kamati inayoshughulikia uundaji wa mdundo wa Taifa imesema itafanya kikao cha pamoja na wadau mbalimbali wa sanaa kwa lengo la kukusanya maoni yao kuhusu namna watakavyotengeneza wimbo mmoja utakaotambulisha mdundo wa muziki wa kitaifa utakaotumiwa na wasanii nchini.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Kedmon Mapana ambapo amesema baada ya kukusanya sampuli za midundo kutoka makabila mbalimbali watachukua maoni kutoka kwa wadau ili kupata yaliyo bora zaidi ambayo yatatumika kutambua mdundo wa taifa.
“Tumekusanya maoni kutoka Kanda ya Kusini, Zanzibar, Kanda ya Kati, Pwani huku tukitarajia kwenda Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa, na tumeanza kurekodi midundo tofauti kulingana na maoni yaliyokusanywa. Sasa tunataka kusikiliza wadau wetu wanasemaje kwa lengo la kuwa na angalau beat mbili au tatu zitakazotumika kama mdundo wa kitaifa,” amesema Mapana.
Mapana amewahimiza wadau wa sanaa na muziki kujitokeza na kutoa maoni yao ili waweze kutengeneza mdundo bora utakaopigwa dunia nzima na kutumiwa na wasanii kama ishara ya utaifa, na kusisitiza kuwa watayarishaji na wapigaji wa muziki