Kamati ya TFF yaiondolea adhabu Singida Big Stars

0
73

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeiondolea Klabu ya Singida Big Stars (SBS) adhabu ya kufungiwa kusajili.

Kamati imesema badala ya adhabu hiyo, klabu imepigwa faini ya TZS milioni moja ambayo inatakiwa kulipwa kabla ya dirisha dogo la usajili kufungiliwa Desemba 15 mwaka huu.

Uamuzi huo umefanywa leo Novemba 29, 2022 na Kamati mara baada ya kupitia hoja za SBS katika maombi yao ya marejeo (review) kuhusu uamuzi wa awali wa klufungiwa kusajili

Taarifa imeeleza kuwa iwapo SBS haitalipa faini hiyo ndani ya muda uliowekwa, adhabu ya kufungiwa kusajili itabaki palepale.

Kamati ilitoa adhabu hiyo kwa Singida Big Stars baada ya kukiuka kanuni za usajili wa wachezaji kwa kusajili wachezaji wenye mikataba na klabu zingine Oktoba 7, mwaka huu

Send this to a friend