Kamati yaundwa kuchunguza matokeo ya Shule Kuu ya Sheria

0
47

Serikali imeunda kamati ya watu saba ili kuchunguza sintofahamu iliyojitokeza kwenye matokeo ya mitihani katika Shule Kuu ya Sheria Tanzania (Law School of Tanzania).

Kamati hiyo itaongozwa na Dkt. Harrison Mwakyembe na imepewa siku 30 kuanzia Oktoba 13 ili kubaini tatizo liko wapi na kutoa majibu juu ya sakata hilo.

Ishara 7 zinazoonesha unatapeliwa katika biashara za kuwekeza

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro leo Oktoba 12, 2022 jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi ikiwa ni siku chache tu baada ya kuripotiwa kwa taarifa za wanafunzi wa shule hiyo kuwa na matokeo mabaya.

“Kuna tatizo ambalo lazima twende mbele tulijue, kama tatizo ni law school tujue, kama tatizo ni wanafunzi wenyewe tujue kama tatizo ni wazazi tujue, tukikaa kwenye chumba hiki hatutajua tatizo,” amesema.

Send this to a friend