Kamati yaundwa kushauri mabadiliko ndani ya majeshi na taasisi za haki

0
58

Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati na Sekretarieti zitakazoshauri namna ya kuleta mabadiliko ya utendaji kazi wenye matokeo bora katika vyombo vya utendaji haki.

Rais amesema hayo katika hafla ya uapisho wa viongozi mbalimbali iliyofanyika Ikulu Chamwino, akieleza kuwa kamati hiyo itaongozwa na Jaji Mstaafu, Chande Othman.

Amesema kamati hiyo itaanza kulifanyia kazi Jeshi la Polisi na baadaye katika majeshi mengine ya ulinzi na vyombo vya utendaji haki.

“Serikali itapitia na kurekebisha miundo, mifumo ya ajira na mafunzo, mifumo ya upandishaji vyeo, madaraka na taaluma za kijeshi,” ameeleza.

Ametaja masuala mengine kuwa ni kutoa mafunzo kwa majeshi ya ulinzi kuhusu matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na mahusiano ya Jeshi la Polisi na taasisi nyingine ikiwemo kanuni na sheria zinazoongoza taasisi hizo.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa ufanisi, na kuimarisha usalama wa raia na mali zao na kuzingatia haki za binadamu

Send this to a friend