Baada ya wananchi mkoani Mwanza kudai kuchukuliwa kwa eneo la makazi ya Isamilo na kupewa vigogo 39 bila ya kupewa fidia yoyote, mmoja wa wadaiwa waliotajwa kumilikishwa eneo hilo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Alphayo Kidata amekanusha kutohusika na madai hayo.
Kidata amesema hajawahi kuomba kuuziwa kiwanja katika eneo hilo hivyo anashanganzwa kusikia jina lake limeandikwa kwenye vyombo vya habari kama mmoja wa vigogo wao.
Aidha, mmoja wa viongozi kutoka Jiji la Mwanza amesema huwa wanawapa viongozi wa Serikali pamoja na wabunge viwanja bila hata wao kujua.
Serikali kutoa mikopo ya kujenga vituo vya mafuta vijijini
Amesema halmashauri nyingi nchini zinafanya hivyo zinapokuwa na miradi mikubwa ya kupima viwanja na kuviuza kwa wananchi, hivyo wanatoa vipaumbele kwa viongozi hao.
“Wakati mwingine hata hao tunaowapa viwanja wanakuwa hawajawahi kufikia huko na huwa tunawapa taarifa baadaye kama wamepewa viwanja na kutakiwa kwenda kuvilipia, na huenda hicho ndicho kiilichofanyika katika sakata hili” amesema.
Chanzo: Nipashe.