Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Droo ya Kampeni ya Mtoko wa Kibingwa kwa msimu wa tano imefanyika na tayari imeibuka na washindi wanne huku kwa mara ya kwanza, katika Kampeni hiyo amepatikana mshindi wa Jinsia ya kike.
Kampuni ya michezo ya ubashiri ya Betika imetangaza washindi wa droo ya kwanza na ya pili kwa msimu huu wa tano na kupatikana washindi hao wanne kutoka mikoa ya Songea, Simiyu, Kagera na Dar es Salaaam.
Aidha, mshindi kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Mariam Mohammed (24) mkazi wa Chamazi amesema anajisikia furaha kushinda katika droo hiyo ya mtoko wa kibingwa kwa msimu wa tano. “Nina kawaida ya kucheza mara kwa mara lakini nilipopigiwa na kupewa taarifa kuwa nimeshinda nilifurahi zaidi.”
Hata hivyo, Mariam amesema siku ya Dabi ya Kariakoo atashangilia timu zote kwa sababu yeye hana timu ambayo anashangilia (Kindaki ndaki) kwenye timu zote mbili. Pia amewashauri wanawake kuweka ubashiri wao kwani michezo ya ubashiri haichagui jinsia .
Mshindi kutoka Mkoa wa Ruvuma, Songea, Constantine Mbele (26) ambaye ni Dereva amesema ameshiriki Kampeni hiyo kwa kuweka ubashiri wake kwa kiasi cha Shilingi 3000 kwa mikeka mitano yenye mechi tatu. “Nimeshiriki sana ubashiri kwenye Kampuni ya Betika na nimeshashinda fedha Shilingi Laki 3 (300,000/-) ambayo nilifanya manunuzi ya mbolea na kununua mahitaji mbalimbali.”
Aidha, Mbele ameeleza shahuku yake kubwa kufika jijini Dar es Salaam kwa sababu hajawahi kufika, huku shahuku yake kubwa kumuona Mchezaji wa Simba SC, Clotous Chama. “Mimi ni shabiki wa Mnyama, Simba SC, na Aprili 16,2023 natarajia makubwa kwenye timu yangu na tutapata ushindi dhidi ya Wapinzani wetu Yanga SC hivyo nategemea zaidi Chama atafunga magoli.”
Pia msimu huu utachukua washindi 100 na utaenda kukamilisha idadi ya washindi 500 wa Kampeni ya mtoko wa Kibingwa ambapo msimu wa kwanza walishinda washindi 400. Kushiriki ubashiri huo ni rahisi kwa kutembelea Tovuti ya www.betika.com au kwa wale wenye Simu za mkononi watabofya *149*16# kwa kuweka dau la Shilingi mia 500 kwa mikeka mitatu.