Kampuni 30 zautaka mradi wa Mwendokasi

0
40

Wakala wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART) umesema kampuni zaidi ya 30 zinawania zabuni ya uendeshaji wa Mradi wa Usafiri wa Haraka (UDART) Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa.

Agizo hilo lililotolewa na Machi 20 mwaka huu limetaka kuwepo umuhimu wa kushirikisha sekta binafsi kutokana na changamoto zilizopo katika utoaji huduma, na kwamba iwapo itashindikana viongozi wa UDART na DART waandike barua za kujiuzulu.

Mtendaji Mkuu wa DART, Dkt. Athuman Kihamia ametaja baadhi ya kampuni hizo kuwa ni kutoka Dubai, Asia, Uingereza na Afrika huku akibainisha kuwa hakuna kampuni iliyoshinda zabuni, na kwamba DART inaendelea na mchakato wa manunuzi.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa UDART ambaye ameteuliwa Machi 9, mwaka huu na Rais Samia Suluhu amesema maagizo ya Waziri Mchengerwa wameyasikia na wanapaswa kuyafanyia kazi.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend