Kampuni ya Bakhresa yaanza uzalishaji wa sukari

0
41

Uzalishaji wa sukari nchini umeimarika baada ya Said Salim Bakhresa Group of Companies (SSBG) kuanza uzalishaji katika kiwanda chake cha Bagamoyo Sugar Ltd.

Mkurugenzi wa masuala ya ushirika wa SSBG, Hussein Sufian amesema mradi huo ambao una awamu tatu, ulianza uzalishaji wenye uwezo wa kufunga kati ya tani 30,000 na tani 40,000 za sukari kwa mwaka, huku tayari wakiwa wamevuna hekta 1,200 za miwa ambayo ililimwa katika awamu ya kwanza.

Bei ya mafuta ya kupikia yaanza kushuka

“Kiwanda chetu kinapanuka, kulingana na upatikanaji wa miwa, kinaweza kufikia uwezo wa uzalishaji wa tani 100,000 kwa mwaka baada ya kukamilika kwa awamu zote tatu,” amesema Sufian, huku akieleza kuwa utatoa ajira 10,000 za moja kwa moja.

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema kukiwa na washiriki wapya katika uzalishaji wa sukari, Serikali katika miaka mitatu ijayo itaziba pengo la upungufu wa bidhaa hiyo ambayo kwa sasa inafikia takriban tani 77,500.

Ameongeza kuwa Serikali ina imani ya kutimiza ndoto ya kuifanya Tanzania kujitegemea ifikapo 2025, na hivyo kukabiliana na uhaba wa sukari unaoendelea sokoni.

Send this to a friend