Kampuni ya Bia ya Serengeti Yazidi Kuonesha Uaminifu wa Kuendeleza Ukuaji wa Viwanda kwa Ushirikiano na Wizara ya Viwanda na Biashara

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) jana imekutana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Judith Kapinga, katika mkutano wa kimkakati ulioelekezwa kwenye kuimarisha ajenda ya viwanda nchini Tanzania, kukuza ongezeko la thamani, na kupanua fursa za kiuchumi. Uwakilishi wa SBL uliongozwa na Mkurugenzi wa Fedha, Emmanuel Kyarwenda, pamoja na wakuu wa idara za kampuni.

Mjadala ulijikita katika nafasi muhimu ya sekta binafsi katika kusaidia maendeleo ya viwanda nchini Tanzania kupitia uwekezaji endelevu katika utengenezaji wa ndani, kuimarisha minyororo ya ugavi wa ndani, na kuendesha ongezeko la thamani katika sekta muhimu za uchumi.
Kama moja ya wazalishaji wakuu nchini Tanzania, SBL inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye taswira ya viwanda ya taifa kupitia vituo vyake vya uzalishaji vilivyo Moshi, Dar es Salaam, na Mwanza, ambavyo vinaendelea kuimarisha uwezo wa taifa katika uzalishaji huku vikitoa ajira na fursa za kiuchumi katika sekta mbalimbali.

Kupitia operesheni zake, SBL inaajiri ajira rasmi na na zisizo rasmi kwa watu zaidi ya 800, huku takriban watu 140,000 wakinufaika kupitia minyororo yake ya thamani, ikiwemo wasambazaji, wasafirishaji, wauzaji, na washiriki katika sekta ya huduma za migahawa na hoteli.
Sehemu muhimu ya mjadala ilikuwa uwekezaji endelevu wa kampuni katika ununuzi wa ndani. SBL inapata takriban tani 20,000 za nafaka kutoka ndani ya nchi , zinazowakilisha karibu asilimia 80 ya mahitaji yake ya malighafi, na kuchangia zaidi ya TZS bilioni 15 kila mwaka kwenye minyororo yake ya kilimo. Kwa mazao ya shayiri, mahindi, na mtama yanayolimwa nchini na kutumika katika uzalishaji wa bia, kampuni inaendelea kuimarisha minyororo ya ugavi wa ndani, kupunguza utegemezi wa bidhaa za nje, na kuchangia kwenye ajenda pana ya viwanda ya Tanzania.
Wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Fedha wa SBL, Emmanuel Kyarwenda, alisema:
“Kampuni ya Bia ya Serengeti inaendelea kuunga mkono maendeleo ya viwanda nchini Tanzania. Kupitia uwekezaji wetu katika utengenezaji wetu wa bidhaa wa ndani, ongezeko la thamani, na mtandao thabiti wa usamabazaji wa huduma zetu nchini, tunachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi huku tukitengeneza fursa kwa Watanzania katika kila kiungo cha mnyororo wetu wa thamani. Wakati Tanzania ikielekea kutimiza ndoto yake ya kuwa na uchumi wa dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050, sekta binafsi itaendelea kuwa na nafasi muhimu, na tunajivunia kuwa sehemu ya mchakato huu wa mabadiliko.”

Mheshimiwa Judith Kapinga, Waziri wa Viwanda na Biashara, alithamini jitihada za kampuni akisema:
“Serikali inathamini sana washirika wa sekta binafsi kama Kampuni ya Bia ya Serengeti, ambao wanachangia moja kwa moja katika maendeleo ya viwanda kupitia utengenezaji wao wa bidhaa wanaofanyia ndani ya nchi, ongezeko la thamani, na utengenezaji wa ajira. Ushirikiano wa karibu na endelevu kati ya serikali na sekta binafsi ni muhimu ili kuimarisha uzalishaji wa ndani, kupanua minyororo ya ugavi, na kufungua fursa za ukuaji wa uchumi endelevu.”

Mkutano huo ulimalizika kwa kujitolea pamoja kuendeleza ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika kukuza ukuaji wa viwanda, kuimarisha uzalishaji wa ndani, na kupanua ongezeko la thamani katika uchumi wa Tanzania.

About SBL:
Incorporated in 1988 as Associated Breweries, SBL is the second-largest beer company in Tanzania, with its beer brands accounting for over 30% of the market by volume. SBL has three operating plants in Dar es Salaam, Mwanza, and Moshi.
Since the creation of SBL in 2002, the business has grown its portfolio of brands year on year. The majority stake acquisition by EABL/Diageo in 2010 has seen increased investment in international quality standards leading to greater job opportunities for the people of Tanzania.
SBL Brands have been receiving multiple international awards and include Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Serengeti Lemon, Pilsner Lager, Kibo Gold, Guinness stout and Smooth and Senator. The company is also home to world renowned spirits such as Johnnie Walker, Smirnoff Vodka, Gordon Gin, Captain Morgan Rum and Baileys Irish Cream.
For further information contact:
Rispa Hatibu,
SBL Communications and Sustainability Manager
Tel: +255 685260901
Email: Rispa.Hatibu@diageo.com









