Kampuni ya Marekani yatangaza mafaniko ya awali ya chanjo ya corona

0
38

Kampuni ya kibiolojia ya Marekani, Moderna, imeripoti matokeo chanya ya awali ya chanjo ya kukabliana na virusi vya corona kufuatia majaribio ya awali yaliyofanyika kwa watu wachace waliojitolea.

Chanjo hiyo, mRNA-1273, imeonesha kuzalisha kinga ya mwili kwa watu waliotumia. Hata hivyo matokeo kamili ya awamu ya kwanza ya chanjo hiyo iliyohusisha watu 45 hayajatolewa.

Kampuni hiyo imesema kwamba chanjo hiyo ilikuwa salama kwa binadamu, na kuongeza kuwa kinga iliyozalishwa ilikuwa na ukubwa sawa na madhara yaliyotokana na maambukizi ya virusi.

Watu 45 waliohusika katika majaribio ya chanjo hiyo waligawanywa katika makundi matatu ya watu 15 kila kundi, na kupewa dozi tatu tofauti za chanjo.

Kampuni hiyo imesema kuwa awamu ya pili itakayohusisha watu wengi zaidi itaanza karibuni, huku awamu ya tatu ambayo ndiyo muhimu itakayothibitisha uimara wa dawa hiyo itaanza Julai.

Moderna imesema kuwa majaribio tofauti yalifanywa kwa panya na kuonesha kuwa chanjo ilizui virusi kuongezeka kwenye mapafu yao.

Send this to a friend