Kampuni ya Tigo yajiandaa kuorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la Dar Es Salaam

0
47

Kampuni za mawasiliano ya simu nchini Tanzania ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla. Sekta ya mawasiliano ya simu huchangia 5.2% ya Pato la Taifa (GDP), ambapo huzalisha takribani TZS 5.7 trilioni.

Simu za mkononi pia zimekuwa na nafasi kubwa katika mfumo wa malipo ya serikali kwa njia ya kielektroniki (e-government), na pia zimesaidia taasisi nyingi za umma kushirikiana moja kwa moja na wananchi kwa njia ya huduma za fedha kwenye simu au jumbe fupi (SMS).

Kwa mujibu wa matakwa ya sheria nchini, kampuni za mawasiliano zinatakiwa korodhesha angalu 25% ya hisa zao katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Katika mahojiano ya hivi karibuni na jarida la Forbes, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo alieleza kuwa Tigo ipo katika hatua za mwisho kukamilisha korodhesha hisa zao kwa ajili ya mauzo ya awali (IPO).Kwa mujibu wa Simon Karikari, kampuni inashauku ya kukamilisha hatua hiyo kwa sababu kuorodhesha hisa hizo kutatoa fursa kwa wazawa kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hiyo. Hii itasaidia kuongeza umiliki wa kampuni na Watanzani ndani ya nchi.

Kabla kampuni hiyo haijaorodhesha hisa zake, ina mpango wa kuunga na kampuni nyingine ya Zantel. Inaaminika kuwa muungano huo utaboresha huduma zinazotolewa na Tigo pamoja na Zantel kwa wateja wao.

Muungano wa kampuni hizi utatengeneza mtandao imara zaidi kwa ajili ya wateja wa pande zote mbili, lakini pia itawaruhusu wateja wa Zantel kuweza kutumia huduma za kiwango cha juu za Tigo.

Kubwa zaidi, soko la mawasiliano lililoimara litakuwa na faida kubwa sana kwa wateja, kwani itakuwa na maana kwa, kampuni hizo zitaweza kutumia fedha zao kuwekeza kwenye teknolojia na utoaji huduma kwa wateja.

Ni jambo jema na lenye kufurahisha sana kuona kampuni zetu zikifanya kazi kwa ajili ya manufaa ya wateja, na pia kuwezesha wazawa kuwa sehemu ya wamiliki kupitia uuzwaji wa hisa (IPO).

Send this to a friend