Kampuni ya xAI yaununua mtandao wa X

0
19

Mfanyabiashara Elon Musk amesema kampuni aliyoianzisha ya matumizi ya akili mnemba iitwayo xAI imeununua mtandao wa kijamii wa X [zamani Twitter].

Musk aliununua mtandao wa Twitter mwaka 2022 kwa thamani ya Dola bilioni 44 sawa na shilingi trilioni 116.6 za Kitanzania.

Kupitia chapisho lake kwenye X siku ya Ijumaa, Musk amesema muamala huo umefanyika kwa kutumia hisa badala ya fedha taslimu, ambapo xAI imepewa thamani ya dola bilioni 80, huku X ikithaminiwa kwa dola bilioni 33.

Marekani yapanga kusitisha ufadhili kwa Shirika la chanjo

xAI ni kampuni ya akili bandia (AI) ya Marekani iliyoanzishwa na Elon Musk mwaka 2023. Kampuni hii inafanya kazi kama shirika lenye malengo ya manufaa kwa umma na inalenga kuendeleza mifumo ya AI ya hali ya juu.

Makao makuu ya xAI yako San Francisco, California, na timu yake inajumuisha wataalamu wa AI waliowahi kufanya kazi kwenye miradi kama GPT na Google DeepMind.

Moja ya miradi maarufu ya xAI ni Grok, chatbot iliyotengenezwa kushindana na ChatGPT ya OpenAI na Google Gemini. Tangu kuzinduliwa, Grok imepata umaarufu mkubwa na sasa imeunganishwa kwenye jukwaa la X.

 

Send this to a friend