Kamwaga aeleza sababu za kuzushiwa kuwa amejiuzulu

0
38



Kaimu Afisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amekanusha taarifa zilizozushwa kwamba amejiuzulu nafasi hiyo.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Kamwaga ameeleza kushangazwa na taarifa hizo zinazosambazwa na waandishi wenzake, wengine wazoefu, kuhusu yeye kubwaga manyanga Simba.

“Mimi bado nipo Simba. Tena bado nipo sana. Uongo huu dhidi yangu na Simba SC upuuzwe,” amesema Kamwaga.

Amesema taarifa hizo zimezua taharuki isiyo na sababu kwa viongozi, wanachama wenzake na washabiki wa Simba kwa ujumla.

“Baada ya kuona usajili wa aina yake na mipango mikubwa mikubwa ya Simba ikiwa inatekelezwa, wabaya wetu wameibuka na uongo mwingine. Njia ya mwongo ni fupi.”



“Nimepewa majukumu yangu mahususi Simba kwa muda wa miezi miwili na bado kazi hiyo sijaikamilisha. Nimedhamiria kukamilisha majukumu hayo mpaka ukomo wake,” ameongoza.

Taarifa za kujiuzulu Kamwaga zinaadai kuwa amejiuzulu baada ya kutoelewana na waajiri wake waliompa kazi wiki chache zilizopita.

Kamwaga aliteuliwa kushika wadhifa huo baada ya Haji Manara kuondoka klabuni hapo.

Send this to a friend