Kanisa lahusishwa na mauaji ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Japan

0
12

Serikali ya Japan imeiomba mahakama iamuru kufutwa kwa kanisa ambalo shughuli zake zimehusishwa kuwa sababu ya kuuawa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Shinzo Abe mwaka jana.

Mauaji ya Abe yalipelekea kanisa hilo linalojulikana kama ‘Moonies’ kuwekwa katika uangalizi baada ya mtu aliyemshambulia anayetambuliwa kama Tetsuya Yamagami kudai kanisa hilo lilimfilisi mama yake kwa kuchukua michango mingi na kumlaumu Abe kwa kuliendeleza.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Hirokazu Matsuno, amesema tayari serikali imewasilisha ombi hilo mahakamani na iwapo itaidhinishwa, kanisa hilo litafutiwa hadhi ya kisheria, lakini bado litaruhusiwa kuendelea na shughuli zake nchini Japan japokuwa litapoteza faida za kodi.

Israel: Wanafunzi wawili wa Kitanzania bado hawajulikani walipo

Kanisa hilo limejibu katika tovuti yake kwamba, uamuzi uliochukuliwa na serikali kutaka kuvunjwa kwa kanisa hilo si wa haki na kuapa kupinga kesi hiyo mahakamani.

Send this to a friend