Kanisa lamshtaki DC Nyamagana, Mahakama yampa siku tano

0
57

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imempa siku tano Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi kuwasilisha mahakamani kiapo kinzani kuhusu shauri la madai ya ugomvi wa kanisa ambalo umiliki wake unagombewa na uongozi wa kanisa la Assemblies of God Gospel Church International (AGGCI) na kanisa la Evangelical Assemblies of God in Tanzania (EAGT).

Mchungaji wa AGGCI, Benson Kitonka ambaye ndiye mleta maombi kupitia wakili wake, Gibson Ishengoma amesema pamoja na mahakama kutoa amri Desemba 20, 2023 kwa mkuu wa wilaya ikimtaka asitishe uamuzi alioutoa wa kuzuia ibada kufanyika ndani ya kanisa hilo, amri hiyo haijatekelezwa.

Hivyo, mleta maombi kupitia wakili wake ameiomba mahakama kuu itoe maelezo kwa DC Makilagi kuwasilisha utetezi wake kwanini hajatekeleza amri ya mahakama hiyo, iliyomtaka awaruhusu waumini wa AGGCI kusali kwenye kanisa hilo.

Hata hivyo, wakili wa Serikali, Sabina Yongo ameieleza mahakama kuwa mjibu maombi (DC Makilagi) alishindwa kuwasilisha kiapo kinzani kwa sababu yupo mapumzikoni, hivyo ameiomba mahakama kumpa muda ili kutekeleza amri hiyo.

Send this to a friend