Kanuni mpya za LATRA kuwaadhibu abiria wanaokiuka sheria za barabarani

0
42

Abiria wanaoshiriki katika uvunjaji wa sheria na kanuni zinazoongoza vyombo vya moto na usalama barabarani wataanza kupata adhabu baada ya rasimu ya kanuni mpya zinazoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) kukubaliwa na wadau.

Hivi sasa abiria watakaokwenda kinyume na sheria watapata adhabu tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo adhabu ilitolewa kwa madereva  na wamiliki wa vyombo vya usafiri.

LATRA imependekeza abiria ashirikishwe wakitolea mfano kwa wanaopanda watu watatu kwenye pikipiki moja (mshikaki), abiria kukaa mbele na dereva kwenye bajaji au pale itakapobainika kumshawishi dereva kuongeza mwendo.

Mapendekezo hayo yaliungwa mkono na wadau katika kikao kilichofanyika  jijini Dar es Salaam wakati Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ilipokuwa ikipokea maoni ya wadau kuhusu rasimu za kanuni  hizo mpya.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki Daladala mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA), Shifwaya Lema amesema wangependa dereva  anapofanya makosa aadhibiwe yeye na si mmiliki wa chombo.

Send this to a friend