Kaoneka alalamika Mandonga kuwa maarufu kuliko yeye

0
70

Bondia wa ngumi nchini, Shabani Kaoneka amewalalamikia waandishi wa habari kuwa wanaegemea upande wa bondia Karim Mandonga na kumpa fursa mbalimbali licha ya kuwa yeye ndiye mshindi wa pambano.

Ameyasema hayo katika mahojiano na chombo cha habari baada ya mechi ya Simba SC dhidi ya St. George SC siku ya Simba Day katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Yule amepata bahati kuliko mimi, kwa sababu hata nyie waandishi wa habari wakati mwingine mnakuwa wanafiki, mkimuona Kaoneka kaalikwa kwenye sehemu ndio mnasogea lakini mbona Mandonga mnamfanyia ‘suprise’ nyingi mnamuita twende sehemu hii na hii,?” amehoji Kaoneka.

Wanaume wanaotafuta ‘six pack’ watahadharishwa kuota matiti

Kaoneka ameongeza kuwa “mimi niliyeshinda nakuwa masikini, aliyepigwa anakuwa tajiri, mimi najisikiaje?

Julai 30 bondia Karim Mandonga alipoteza mchezo dhidi ya Shabani Kaoneka katika raundi ya 4 kwenye uwanja wa Majimaji, Songea

Send this to a friend