Kapinga: Taasisi zote zinazotoa huduma za kijamii zitaunganishiwa umeme

0
42

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijin (REA) tayari wamejidhatiti kuhakikisha kuwa taasisi zote zinazotoa huduma za kijamii kama shule na vituo vya afya pamoja na nyumba za ibada zinafikishiwa umeme.

Akizungumza wakati akiwasha umeme katika Shule ya Sekondari Nyasa iliyoko Kijiji cha Chimate wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, amesema uwepo wa umeme shuleni umesaidia kuongeza ufaulu kwani wanafunzi wamekuwa wakipata muda wa kujisomea hata usiku tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya miradi ya kusambaza umeme vijijini inayotekelezwa na REA haijaanza.

“Sisi kama Wizara ya Nishati ni kuhakikisha tunaongeza tija katika taasisi hizi zinazotoa huduma kwa kufikisha umeme. Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu anahangaika usiku na mchana kutafuta fedha za kuboresha maisha ya Watanzania kila siku na kazi yetu kubwa ni kuhakikisha taasisi na maeneo yote yenye umuhumi yanafikiwa na umeme.

Aidha, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Eng. Robert Dulle amesema Mkoa wa Ruvuma una jumla ya vijiji 554 na mpaka kufikia Julai 2024, vijiji 542 sawa na asilimia 97.8 vimepata huduma ya umeme kupitia miradi inayotekelezwa na REA na kwa Wilaya ya Nyasa kuna jumla ya vijiji 84 ambapo vyote vimepata umeme.

Send this to a friend