Kapinga: TANESCO rekebisheni transifoma ndani ya siku 30 umeme usikatike

0
23

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ametoa siku 30 kwa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wanafanyia kazi dosari na mapungufu yote yaliyopo kwenye mashine umba (transfoma) zenye kasoro ili kuendelea kutoa huduma ya umeme wa uhakika nchini.

Ametoa agizo hilo leo Januari 26 jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa Kituo cha kupoza umeme cha Mbagala pamoja na njia ya msongo wa Kilovoti 132 kutoka Kituo cha kupoza umeme cha Ilala kwenda Kurasini kwa kutumia waya zinazopita ardhini.

“TANESCO nawapa siku 30 muhakikishe mnafanya marekebisho ya miundombinu ya umeme zikiwemo mashine umba kwa kuzifungia vifaa vinavyostahili ili wananchi wapate umeme wa uhakika bila kukatika ovyo katika baadhi ya maeneo hapa nchini.

Watumishi wa afya wapigwa marufuku kuchati kazini

Haiwezekani Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anahangaika usiku na mchana kutafuta fedha za kuwaletea maendeleo wananchi halafu tunashindwa kununua kifaa cha laki tano kwenye transifoma tuliyonunua kwa zaidi ya milioni 10. Hii sio sawa kabisa,” amesema Kapinga.

Ameongeza kuwa watendaji wa TANESCO wanahitaji kubadilika na kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia taaluma zao ili waendelee kulinda miundombinu ya umeme ambayo serikali inawekeza fedha nyingi kwa lengo la kufikisha huduma bora ya umeme kwa wananchi.

Send this to a friend