Karani ajiua saa chache kabla ya Sensa, aacha ujumbe

0
40

Mmoja kati ya makarani wa Sensa wilayani Igunga, mkoani Tabora aliyefahamika kwa jina la Edmund Zakayo, mwalimu wa Shule ya Msingi Buchenjegele amejinyonga usiku wa kuamkia siku ya Sensa kutokana na mgogoro wa familia.

Marehemu ameacha ujumbe uliosomeka kuwa asilaumiwe mtu yeyote kutokana na tukio la kujinyonga kwake, kwa kuwa ni mgogoro unaohusisha familia yake hivyo asihusishwe mtu yeyote.

Makarani wawili wa Sensa waporwa vishkwambi vya Sensa

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Dkt. Batilda Buriani amesema baada ya Mkuu wa Wilaya kufika nyumbani kwa marehemu walikuta vifaa vyote vya Sensa vipo pamoja na barua hiyo.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali imesikitishwa na tukio hilo la Karani kuchukua uamuzi wa kukatisha uhai wake, na kuomba kuwepo na huduma za ushauri katika maeneo mbalimbali ili kuepusha wimbi la watu kujiua.

Send this to a friend