Kardinali Rugambwa ahimiza umoja na mshikamano kwa Watanzania

0
48

Kardinali Protase Rugambwa amewataka Watanzania wawe tayari kujenga na kudumisha utamaduni wa upendo na mshikamano wa kitaifa pamoja na watu wengine, hata ambao si Watanzania, kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa Kanisa la Kisinodi.

Kardinali Rugambwa ametoa wito huo akizungumza na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Italia, baada ya kusimikwa kuwa Kardinali na Baba Mtakatifu Francisko, hafla iliyofanyika Septemba 30, 2023 mjini Vatican, ambapo ni miongoni mwa Makrdinali wapya 21.

Ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wageni nchini Tanzania akisema “Tanzania kumenoga, karibuni nyote.”

Aidha, amewaomba kuendelea kumwombea ili atumike vyema katika maisha na utume wake kama Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Tabora na kama Kardinali.

Ng’ombe alizotoa Rais Samia mradi wa BBT zaibwa

Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Mahmoud Thabit Kombo, Balozi wa Tanzania nchini Italia amefikisha pongezi za Rais Samia Suluhu anatoa kwa Kardinali Protase Rugambwa, ambaye ameandika historia kwa kuwa Kardinali wa tatu kutoka Tanzania.

“Naungana na Watanzania wote kukuombea kheri, afya njema, na mafanikio katika utumishi wako,” aliandika Mheshimiwa Rais Samia katika ujumbe wake kwa pongezi kwa Kardinali.

Send this to a friend