Karia: Milioni 500 hutumika kugharamia mchezo mmoja wa timu ya Taifa

0
41

Rais wa TFF, Wallace Karia amesema gharama zinazotumika katika mchezo mmoja wa timu za taifa ni takribani TZS milioni 500, gharama zinazojumuisha usafiri, malazi, chakula n.k.

Aidha, amesema chanzo kikuu cha  mapato ya gharama zinazotumika kuhudumua timu za taifa ni kutoka FIFA, CAF, wadau mbalimbali pamoja na harambee iliyofanywa na Serikali hivi karibuni.

“Katikati hapa Serikali nayo ilijaribu kufanya harambee ingawa mimi nina mtazamo tofauti kidogo na hizi harambee, saa nyingine zinatupoteza lakini bado tunaendelea kuzungumza na Serikali tuangalie kwamba tunazifanya katika utaratibu gani,” amesema.

Send this to a friend