Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia amekanusha madai ya kuhusishwa kwamba yeye ni mwanachama wa Simba.
Akizungumza katika mahojiano kupitia mtandao wa Zoom, Karia amesema mpira wa miguu unaongozwa na viongozi ambao wametoka kwenye mpira wa miguu ambao pia wana vilabu vyao, hivyo kitu kikubwa kinachotakiwa ni kiwango kikubwa cha maadili ili kutenda haki.
Timu itakayoshindwa kufika uwanjani kupokonywa alama 15
“Mimi nikiri kwamba mimi wala siyo mwanachama wa Simba, mimi ni mwanachama wa Coast Union na nilikuwa kiongozi wa Coast Union, na lile tukio ni la miaka mingi sana wakati bado ni Makamu. Niliagizwa na Rais wangu Malinzi niende nikamuwakilishe kwenye siku ya Simba Day,” amesema.
Aidha, Karia ameeleza kwamba vitu vinavyozungumzwa na propaganda zinazofanyika havina msingi ukilinganisha na utendaji wake wa kazi.’