Karia: Zawadi ya milioni 188 ya timu ya U15 itajengea miundombinu

0
54

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema fedha za zawadi za michuano ya vijana pamoja na ile ya shule (School Championship) zimeelekezwa kujenga miundombinu na sio za kugawana kwa mujibu wa CAF na Motsepe Foundation ambao wanatoa zawadi za mashindano hayo.

Ameyasema hayo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa TFF mkoani Iringa wakati akitoa ufafanuzi baada ya kuwepo kwa taarifa za wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 15 kupewa posho ya TZS 20,000 na kunyang’anywa jezi baada ya kumalizika kwa mashindano nchini Uganda yaliyowapa ushindi wa nafasi ya tatu na kupata zawadi ya TZS milioni 188.

Rais Samia aitaka TFF kutenga pesa za inazokusanya kukarabati viwanja

“Mashindano ya School Championship haya yamechezwa ni msimu wa pili, na haya yanadhaminiwa na Motsepe Foundation, na Motsepe kasema hela yake kahangaika kuitafuta, hataki hela yake igawiwe, anataka hela yake ikajenge miundombinu,” ameeleza.

Kuhusu kunyang’anywa jezi kwa vijana hao, Karia amesema kila kitu kina utaratibu wake na kwamba “wangewezaje kuwapa jezi wakati mashindano mengine yanaendelea.”

Send this to a friend