Katibu Mkuu Mstaafu apinga kuandikwa katiba mpya

0
50

Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Abdurhamid Yahya Mzee amesema hakuna haja ya kuandikwa katiba mpya na badala yake iliyopo ifanyiwe marekebisho katika vipengele vyenye utata.

Ameyasema hayo jana baada ya kuwasilisha maoni yake kwa kikosi kazi cha ukusanyaji maoni kuhusu masuala ya demokrasia kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Chuo kikuu chapiga marufuku mavazi meusi

“Mimi maoni yangu kwa ujumla mchakato uendelee pale ulipoishia lakini pale ambapo kuna vipengele ambavyo vilileta mvutano, vifanyiwe marekebisho na zaidi vipelekwe kwa wananchi ili waweze kuvijadili” amesema.

Mzee amesisitiza kuwa, hakuna haja ya kuanza upya mchakato huo lakini ni muhimu zaidi wananchi wapewe fursa ya kutoa maoni yao kama kuna kasoro au changamoto yoyote.

Send this to a friend