
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema linamshikilia Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Rungwe na Makamu Mwenyekiti Hamasa Taifa, Award Karonga, mkazi wa Katumba kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwemo uchochezi.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema mtuhumiwa alikamatwa Januari 29, 2026 saa 4 asubuhi maeneo ya Mtaa wa Katumba, Kata ya Ibighi, Tukuyu wilayani humo.
Aidha, Jeshi la Polisi limesema upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.







