Kauli ya Benki ya Dunia kuhusu hatma ya Wanafunzi wanaoacha shule Tanzania

0
17

Benki ya Dunia (WB) imesema inaunga mkono uamuzi wa Serikali ya Tanzania kuendeleza elimu mbadala kwa wanafunzi wote walioacha shule kutokana na sababu mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Sera za Maendeleo na Ubia wa Benki ya Dunia, Prof. Mari Pangestu alipofika Ikulu jijini, Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan.

Prof. Pangestu ameonesha utayari wa benki hiyo kusaidia Mfumo wa Ekolojia ya kidijitali kuleta ufanisi katika matumizi ya TEHAMA na ameipongeza Tanzania kwa kutekeleza miradi mbalimbali wanayoifadhilina katika kiwango cha juu na kusema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano.

Rais Samia ametumia mazungumzo hayo kumueleza mkurugenzi huyo utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha zinazotolewa na Benki ya Dunia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule, vituo vya afya, ufanisi katika matumizi ya TEHAMA na miradi ya kikanda.

Send this to a friend