Kauli ya CCM kuhusu waliotangaza nia ya kugombea mitandaoni

0
45

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewaonya wanachama wake wanaochapisha mabango na vipeperushi kwenye karatasi au mitandaoni vyenye kuonesha kuwa wanakusudia kugombea nafas fulani kuacha mara moja kwani ni ukiukwaji wa taratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchakato wa uteuzi wa wagombea Urais, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa mchakato wa kuchukua fomu za kuanza kugombea unaanza Jula 14, 2020, hivyo wale wanaojitangaza wenyewe wamekiuka taratibu.

Aidha, ameziagiza kamati za maadili za chama hicho kwenye ngazi za kata, wilaya na mikoa kuwakemea wale wote walioanza utaratibu huo mapema, na wale watakaokaidi watashughulikiwa kwa namna nyingine.

Send this to a friend