Kauli ya serikali kuhusu wafanyabiashara kuuza mahindi nje ya nchi

0
39

Serikali imesema haijazuia mfanyabiashara yeyote kuuza mazao yake nje ya nchi, na kwamba mkulima wa nchi hii wajibu wake ni kulima, kuvuna, kuhifadhi na kuuza kwa kuwa hiyo ndio biashara yake.

Amesema hayo wakati akizungumza katika ziara ya kikazi wilayani Mpanda mkoani Katavi baada ya kukagua kituo cha kununulia mahindi cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

“Hivyo kama yupo ambaye amazuiwa kuuza mazao yake nje ya nchi wizara inamkaribisha na watampa ushirikiano kwani vibali vyote vya kusafirisha mazao nje ya nchi wanatoa vibali bure ili mradi awe leseni ya kufanya biashara hiyo.

“Serikali imeanza utaratibu wa kujenga na kukodi maghala katika nchi ambazo zina masoko ya mazao kama vile Sudan Kusini, DRC Congo, Kenya, tunaenda kuweka maghala katika nchi hizo ili Bodi yetu ya Mazao Mchanganyiko (CPB) na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) waweke mazao hayo kwenye maghala hayo na kuyauza,” amesema.

Bashe ameongeza Rais Samia Suluhu Hassan amejipambanua kuwalinda wakulima wa Tanzania na wanafahamu bei ya pembejeo imepanda katika soko la dunia hivyo njia pekee ya kumlinda mkulima ni kumpa ruzuku ya mbolea au kununua mahindi yake na hiyo ndiyo sababu Serikali inanunua mahindi ili kulinda wakulima wetu.

Send this to a friend