Kegel, aina ya mazoezi yanayosaidia kuimarisha tendo la ndoa

0
81

Kuna aina mbali mbali za mazoezi lakini kuna baadhi ambayo huwa na manufaa ya kiafya inapokuja katika kujamiiana au tendo la ndoa kwa binadamu.

Mazoezi ya mwili ni sehemu muhimu sana ya afya ya mwanadamu na kuyafanya au kutoyafanya kunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa hali ya afya ya mtu.

Mazoezi ni tiba ya magonjwa mengi na hivyo basi madaktari huwasahauri watu kufanya mazoezi kwasababu ya umuhimu wake wa afya.

Daktari bingwa wa viungo vyo mwili Abubakar Ahmad Tsafe wa hospitali kuu ya Farida Gusau katika jimbo la Zamfara kaskazini mwa Nigeria, anaelezea aina mbali mbali za mazoezi zinazoweza kuboresha afya ya viungo vyo uzazi vya wanaume na wanawake.

Daktari huyo anasema kuwa mazoezi ya viungo yanaweza kumsaidia mtu kukabiliana na adha ya kumaliza mapema tendo la ndoa wakati anapojamiiana au kutoridhishwa na tendo hilo, pamoja na matatizo ya kibofu cha mkojo.

Anasema pia mazoezi kwa upande wa wanawake huwasaidia kuimarisha mishipa ya nyonga.

Mazoezi ya Kegel ni nini?
Dkt Abubakar Ahmad Tsafe, anasema mazoezi ya viungo ya aina ya Kegel ni mazoezi ya tiba.

Kegel ni aina ya mazoezi rahisi yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuimarisha misuli ya nyonga na viungo vilivyopo chini yake kwa wanaume na wanawake.

Eneo hili la nyonga pia ni pamoja na katikati ya mifupa miwili ya miguu kunakoshikilia viungo vya uzazi vya mwanamke na mwanaume.

Katika utafiti wa kina kuhusu mazoezi ya Kegel kwa wanaume na wanawake kwa pamoja, jarida la masuala ya afya la Healthline Health linasema kuwa mazoezi hayo husaidia viungo vilivyopo chini ya nyonga kuboresha mawasiliano na udhibiti wa kibofu cha mkojo na pia kuimarisha uwezo wa tendo la ngono.

Mazoezi ya viungo ya Kegel pia hufanyika ili kuimarisha misuli ya chini ya nyonga kwani udhaifu wake unaweza kusababisha udhaifu pia wa kibofu cha mkojo na tatizo la kutoweza kufanya tendo la ndoa na kutoridhika wakati wa tendo hilo.

Dokta Tsafe anasema kuwa wakati unapofanya mazoezi ya Kegel yanakusaidia kuimarisha misuli ya kiuno, kama ni dhaifu.

Faida za mazoezi ya Kegel kwa wanaume
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha majeraha ya maeneo ya chini ya nyonga au kuyadhoofisha kwasababu wakati wanaume wanapokuwa vijana wanakuwa na nguvu lakini kadri umri unavyozidi kuongezeka watapata majeraha ambayo hatimaye yataathiri maisha yao ya kingono.

Kwa mujibu wa jarida la Healthline tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kwa wanaume, mazoezi ya Kegel yamesaidia kupunguza hali za wanaume wanaoshindwa kujamiiana na kuzuwia umalizaji wa tendo la ndoa kwa haraka.

Yameongeza raha ya kujamiiana na haja ya tendo hilo miongoni mwa wanaume.

Dkt Tsafe anasema kwamba mazoezi ya kegel ni mazuri kwani husaidia mzunguko wa damu mwilini ikiwa ni pamoja na katika viungo vya uzazi chini ya nyonga na hujenga neva na misuli, na kuifanya kuwa imara zaidi.

Pia anasema kuwa kwa wale ambao hawawezi kubana mkojo, mazoezi ya kegel yanaweza kuwasaidia sana.

Faida za Kegel kwa wanawake
Kwa wanawake, matatizo mengi yanaweza kusababisha kuharibika kwa neva na kuifanya sehemu ya nyonga kuwa ngumu hususan kutokana na ubebaji wa mimba na kujifungua au matatizo ya kibofu cha mkojo au kupasuka kwa kibofu cha mkojo.

Lakini kwa kufanya mazoezi ya mara kwa mara ya Kegel, madaktari wanasema wanawake wanaweza kuimarisha misuli ya chini ya nyonga na hivyo kuifanya iwe na ufanisi.

Dkt Tsafe anasema mazoezi ya kegel yanaongeza zaidi mzunguko wa damu katika eneo la nyonga na viungo vya mbele vya mwanamke – kwasababu mazoezi yatasaidia kuondoa uchafu bila kuacha uchafu wowote katika kibofu cha mkojo.

“Yatasaidia kuimarisha neva katika eneo lote la chini ya nyonga – na uchafu utakapokwenda kwenye kibofu cha mkojo utatoka wote kabisa kwa njia ya mkojo na hivyo kuzuwia maumivu katika maeneo ya nyonga na chini yake.”

“Mazoezi ya viungo ya Kegel pia humsaidia mwanamke kuongeza hamu ya tendo la ndoa na kumsaidia kuridhika wanapojamiiana ,” anasema daktari.

Unachotakiwa kufanya kabla ya kuanza mazoezi ya Kegel.

Wakati mazoezi yanapoanza, inafaa kwanza utambue chanzo cha neva je zinawasiliana.

Njia nyingine kwa wanaume na wanawake ni kwa kujaribu kubana kibofu cha mkojo au mkojo wakati unapokojoa na kuuachilia mara kwa mara hadi umalizike.

Neva zinazoshikilia mkojo ni za nyonga ambazo mtu anaweza kuzitambua mahala zilipo – zinahitaji kuhamishwa ili kuongeza ubora na uimara wake kwa kufanya mazoezi ya kegel.

Aina za mazoezi ya Kegel
Kuna aina tofauti za mazoezi ya Kegel – inaweza kufanyika wakati mtu amesimama au kwa kuketi au wakati umelala chini.

Aina rahisi zaidi ni ile unayofanya ukiwa umelala chini na kuweka miguu pamoja halafu unajiinua juu huku ukiwa umenyoosha kando mikono na kukunja magoti.

Dkt Tsafe anasema mazoezi ya kegel pia yanaweza kufanyika kwa sekunde kati ya tatu na tano halafu uvute pumzi kisha unyanyue nyonga juu tena.

Wanaume kwa wanawake wanaweza kufanya mazoezi haya.

Kuna Kegel nyingine unayoweza kuifanya huku ukiwa umeketi na kukunja miguu huku mguu mmoja ukiwa umekunjwa juu ya mwingine.

Hii inaweza kufanywa mara kadhaa na kisha kupumzika na kurudia.

Kuna aina nyingine ya Kegel inaweza kufanywa kama kulaza chini tumbo lakini ukiwa umeweka mkono nyuma huku ukiwa umeshikilia miguu na mikono.

Daktari anasema kwamba unapoelewa mazoezi ya Kegel unaweza kuyafanya wakati wowote na mahala popote-ndani ya nyumba au katika eneo tulivu kazini.

Unaweza kufanya mazoezi haya mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, au wakati unapokuwa na muda.

Na kuna aina nyingi za mazoezi ya Kegel ambayo mtu anaweza kuyafanya kama unafahamu ilipo misuli ya kiuno chako.

Chanzo: bbcswahili

Send this to a friend