Kelvin John asajiliwa KRC Genk ya Ubelgiji

0
19

Mshambuliaji kinda wa Tanzania, Kelvin John ‘Mbappe’ (18) amesajiliwa na KRC Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka mitatu, hadi mwaka 2024, ambapo ataweza kuongeza mkataba kwa misimu miwili.

Hadi karibuni, Kelvin alikuwa Brooke House Football Academy iliyopo Leicester nchini Uingereza, ambapo ilimbidi kusibiri atimize miaka 18 (ametimiza mwezi huu) ili aweze kusajiliwa kucheza soka la kulipwa Ulaya.

Mwanasoka huyo ni machachari kutokana na nguvu na kasi aliyonayo ambapo alijizolea umaarufu sana katika fainali za AFCONU17, wakati huo akiwa na miaka 15.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, ambaye amewahi kukipiga Genk, ndiye aliyefanikisha safari ya ‘Mbappe’ kufika klabuni hapo.

Klevin anaanza maandalizi ya msimu na kikosi cha Genk chini ya kocha John Van de Brom, huku akitadhamiwa kufanya makubwa.

Send this to a friend