Kenya: Amuua mpenzi wake akidai aligeuka mzimu na kutaka kumla

0
45

Mwanamume mwenye umri wa miaka 59, Wangethi Chege amejisalimisha polisi katika eneo la Kasarani, Kaunti ya Nairobi baada ya kudaiwa kumuua mpenzi wake huko Zimmerman akidai kuwa mpenzi wake aligeuka mzimu.

Kulingana na Mkuu wa Polisi eneo la Kasarani, Anthony Mbogo, mshukiwa wa mauaji alifika katika kituo cha polisi na kuwataka maafisa kwenda kuchukua mwili wa marehemu.

Mkuu wa polisi amesema mshukiwa alisema alikutana na marehemu katika sehemu za starehe na kumpeleka nyumbani kwake, kisha alimdunga marehemu kisu mara kadhaa katika maeneo mbalimbali  ya mwili akidai alikuwa amegeuka mzimu na yeye alikuwa akijitetea.

Zingatia mambo haya 6 unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza

“Alisema yule dada aligeuka akawa kama mzimu, ama zimwi na likaanza kufanya kama linataka kumla, lakini sisi tuliona kama tu anajitetea,” ameeleza Mkuu wa Polisi.

Wakati huo huo maafisa wa polisi walipata visu viwili vinavyoaminika kutumiwa na mshukiwa kutekeleza uhalifu huo na kueleza kuwa mwili wa marehemu unasubiri kufanyiwa uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi akisubiri kufikishwa mahakamani.

 

Send this to a friend