Kenya: Amuua mwanaye na kumficha ndani kwa miezi mitatu

0
49

Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 34 anayedaiwa kumuua mtoto wake mchanga aliyejifungua Julai 16 mwaka huu na kuuficha mwili ndani ya nyumba yake kwa zaidi ya miezi mitatu.

Kesi hiyo ilifikishwa polisi na binti wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 14, ambaye alidai nyumba yao iko katika hali mbaya kutokana na harufu mbaya isiyovumilika.

Baada ya kukagua nyumba hiyo, Maafisa wa Polisi walipata mabaki ya mtoto huyo kwenye ndoo ya plastiki iliyofichwa chini ya kitanda.

Akithibitisha kisa hicho Kamanda wa Polisi Kaunti Ndogo ya Kajiado, Daudi Loronyokwe amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi ikiwemo kuchunguza hali ya akili ya mtuhumiwa, na kwamba mwanamke huyo atafikishwa mahakamani Jumatatu Oktoba 31, 2022.

Kamanda Loronyokwe amewataka wazazi kutafuta msaada endapo hawana uwezo wa kuwahudumia watoto wao badala ya kufanya vitendo hivyo viovu.

Send this to a friend