Kenya: Arejea nyumbani baada ya familia yake kuzika mtu mwingine

0
36

Kumetokea hali ya sintofahamu katika kijiji cha Kamukuywa eneo Bunge la Kimilili kaunti ya Bungoma nchini Kenya baada ya mwanamume aliyedhaniwa kuwa amefariki na kuzikwa kujitokeza.

Mwanamume huyo anayejulikana kwa jina Wanjala, alidhaniwa kuuawa na mwili wake kukatwakatwa kiasi cha kutotambulika.

Familia ilienda kuutambua mwili huo katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Webuye mwaka 2021 na walidhani ni wa jamaa yao, kisha mwili huo ulitolewa na kufanyiwa mazishi. Lakini imebainika kuwa familia  ilizika mwili wa mtu mwingine.

Baada ya Wanjala kurejea nyumbani Agosti 29, mwaka huu na kudai kuwa alisafiri nje ya nchi, familia hiyo ilikumbwa na mshtuko huku mama yake Wanjala akidai mwanaye alikuwa akisafiri mara kwa mara nje ya nchi kwa muda wa miezi miwili, lakini mnamo 2019 aliondoka na hakurudi.

Aidha, Mkuu wa Polisi wa Kimilili, Mwita Maroa amewataka wakazi kuwa waangalifu wanapotambua miili ya wapendwa wao.

 

Send this to a friend