KENYA: DJ Brownskin adaiwa kumrekodi mkewe akinywa sumu hadi kufariki 

0
44

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii,  Jumapili  Aprili 02, 2023 imeonekana video ikimuonesha DJ Brownskin akimrekodi mke wake, Sharon Njeri Mwangi akidaiwa kumeza sumu kabla ya kufariki.

Katika video hiyo ya dakika saba, mchumba wake ameonekana akituma ujumbe wake wa mwisho kwa familia yake.

Wakati video ikiisha, imeonesha Njeri akiwa chini huku mtoto wao akikimbilia upande wa mama yake akimsihi DJ Brownskin ampe maziwa.

Akizungumza na Kenyans.co.ke, Wakili wa Kikatiba, Bobby Mkangi, amebainisha kuwa kesi hiyo haikuwa na vigezo vya kisheria lakini imechukuliwa kuwa ya kimaadili zaidi.

Wapelelezi wanachunguza eneo la tukio nchini Kenya.

Hata hivyo, amebainisha kuwa maswali muhimu yaliulizwa kuhusiana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na matukio gani kabla ya video kurekodiwa.

Pia mwanasheria huyo amejiuliza iwapo mke huyo alilazimishwa kuchukua sumu hiyo au DJ Brown Skin alikubali kwa njia yoyote ile.

Mwanasheria huyo amezungumzia suala lingine la kurekodi, ambapo ameeleza kuwa watumiaji wa simu wanapenda kurekodi matukio kama hayo badala ya kutafuta njia ya  kumsaidia mtu aliye katika shida.

Ameongeza kuwa video hiyo itawakilishwa mahakamani kama ushahidi iwapo mahakama itaafiki.

 

Send this to a friend