KENYA: Erick Omondi ahukumiwa kifungo jela

0
38

Mahakama nchini Kenya imemhukumu mchekeshaji maarufu nchini humo, Erick Omondi kifungo cha mwezi mmoja jela au faini ya Ksh.10,000 [TZS 170,524] kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali.

Uamuzi huo umetolewa leo baada ya kukutwa na hatia pamoja na washtakiwa wenzake kwa kwa kufanya mkusanyiko nje ya bunge wakipinga gharama kubwa ya maisha nchini humo.

Katika utetezi wao, Omondi na washtakiwa wenzake walieleza kuwa walikusanyika katika viwanja vya Bunge kuzungumza na Spika wa Bunge ili kushughulikia masuala yenye maslahi kwa taifa.

Tanzania imevuka wastani wa unywaji pombe Afrika

Akijibu hukumu hiyo, Omondi alitumia mtandao wa kijamii wa Instagram kuandika: “Kwa hiyo leo mahakama imenihukumu mimi na vijana hawa kifungo cha mwezi mmoja jela. Tumehukumiwa kwa kupambana na gharama kubwa ya maisha.”

Send this to a friend