Kenya ilivyomfanya Diamond Platnumz kuwa milionea

0
38

Raia wa Kenya wanaongoza kumfanya nyote wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kuwa mmoja wa mastaa wanaoingiza fedha nyingi kupitia mtandao wa YouTube.

Akifanya mahojiano na Billboard 100, Meneja wa YouTube Music Trends, Kevin Meenan amesema watu wengi zaidi wanaotazama video/kazi za Diamond wanatoka nje ya Tanzania, hasa Kenya.

Amesema Kenya inaongoza kutazama kazi za msanii huyo ikifuatiwa na Tanzania kisha Marekani.

Meenan amempongeza Diamond kwa namna anavyojituma katika kazi zake hadi kufikia hapo alipo sasa.

Akitoa siri ya mafanikio yake, Diamond amesema kuwa ni kufanyakazi kwa bidii, kusali na kuwa na mtizamo chanya.

Send this to a friend